Published At: January 27, 2026
Waziri wa Afya Mhe. Mohamed Mchengerwa Januari 26, 2026 amezindua rasmi mfumo wa " Ongea na Waziri", hatua ya kimkakati inayolenga kuisogeza sekta ya afya karibu zaidi na wananchi, kusikiliza sauti zao na kujibu changamoto zao kwa vitendo.<br><br> Uzinduzi huo ni hatua madhubuti ya kuimarisha mawasiliano kati ya wananchi na sekta ya afya, kwa lengo la kuboresha huduma, uwazi na uwajibikaji katika utoaji wa huduma za afya